FOR SPORTS NEWS AND ENTERTAINMENTS UPDATES VISIT THIS BLOG
.

Sunday, December 22, 2013


MANJI: MECHI YA JANA ILIKUWA BONANZA, YANGA TUMEPATA FAIDA SIMBA FURAHA TU


Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji. 
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.

Saturday, December 21, 2013


SIMBA NDIYE MTANI JEMBE,YAIONESHA SOKA YANGA, YAICHAPA 3-1

 Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana.
 Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Yanga.
 Benchi la ufundi la timu ya Simba.
Benchi la Ufundi la Yanga.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu yao.
 Raha ya ushindi.
 Furaha kwa Simba.

 Hamisi Kiiza akitafuta mbinu za kumtoka, Ramadhani singano.
 Ivo Mapunda akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea uwanjani baada ya kuchapwa 3-1 na watani zao wa jadi Simba.
 Juma Kaseja akibembelezwa na Mbuyu Twite baada ya kusababisha 
 Mmoja wa mashabiki wa Yanga akitolewa nje baada ya kuzimia uwanjani.
 Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Simba.
 Wachezaji wa akiba wa Simba  wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho. 
 Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 3-1.
 Wachezaji wa Simba wakimnyanyua juu kocha wao, Zdravko Logarusic mara baada ya kumalizika kwa mchezo maalumu wa Nani Mtani Jembe uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-1.




 Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe akimkabidhi kombe nahodha wa Simba Haruna Shamte.



SIMBA NDIO MTANI JEMBE - TAMBWE APIGA 2 MNYAMA AKIWAUA YANGA 3-1


IVO MAPUNDA NA MASOTI WAANZA DHIDI YA YANGA


Simba line up: Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Henry Joseph, Amisi Tambwe, Said Hamis na Awadh Juma.

MTANI JEMBE: SIMBA VS YANGA - OKWI AANZIA BENCHI - KASEJA AANZA KIKOSI CHA KWANZA

1.Juma Kaseja - 29
2.Mbuyu Twite - 6
3.David Luhende - 3
4.Nadir Haroub "Cannavaro" - 23(C)
5.Kelvin Yondani "Cotton" - 5
6. Athuman Idd " Chuji" - 24
7.Mrisho Ngassa - 17
8.Frank Domayo - 18
9.Didier Kavumbagu - 7
10.Hamis Kiiza - 20
11.Haruna Niyonzima - 8
Subs:
1.Deogratius Munishi "Dida" -30
2.Juma Abdul - 12
3.Oscar Joshua - 4
4.Rajab Zahir - 14
5.Reliants Lusajo - 9
6.Nizar Khalfani - 16
7.Saimon Msuva
8. Hassan Dilunga - 26
9.Jerson Tegete - 10
10.Emmanuel Okwi - 25
11. Said Bahanuzi - 11
12.Hamis Thabit - 22

Sunday, December 21 2013


SIKINDE YAJICHIMBIA BAGAMOYO KUKABILI MSONDO KRISMASI



Na Mwandishi Wetu

HOMA ya pambano la watani wa jadi katika muziki wa dansi nchini kati ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' na Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' litakalofanyika siku ya Krismasi imeanza kupanda kwa bendi hizo kujificha kambini na huku wakipigana vijembe.

Bendi hizo kongwe nchini zinatarajiwa kuonyeshana kazi katika onyesho litakalofanyika kwenye viwanja wa TCC Club Chang'ombe, Temeke Dar es Salaam katika kunogesha sikukuu hiyo ya Krismasi.

Katika kuonyesha wamelipania pambano hilo bendi ya Sikinde tayari imeiendea Msondo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi yao na wamewatahadharisha 'mahasimu' wao hao wasije wakatoa visingizio baada ya kugaragazwa kwenye onyesho hilo.

"Sisi tumeamua kuweka kambi yetu mjini Bagamoyo ambako tutatua viwanja vya TCC kutokea huko ili kuisambaratisha Msondo, na tunataka wajipange sawasawa ili wasije wakatoa visingizio tena kwa maana kama vyombo vipya bendi zote imepewa na Konyagi," Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo alisema.

Milambo alisema mashabiki wa dansi wajitokeze kwa wingi kushuhudia namna gani wanavyowachachafya wapinzani wao hao, ikizingatiwa hawajakutana kwa muda tangu mwaka jana.

Upande wa Msondo kupitia Meneja wao, Said Kibiriti, alisema hawana haja ya kutaja mahali kambi yao ilipo isipokuwa wamejiandaa kuwatoa nishai wapinzani wao siku ya onyesho hilo litakaloanza saa nane mchana.

"Sisi hatuna mchecheto wowote na mpambano huo, tunaendelea kujifua kimya kimya mahali ambapo siwezi kupataja kwa sasa," alisema Kibiriti.

Naye muimbaji anayekuja juu wa bendi hiyo ya Msondo alitokea Sikinde, Athuman Kambi, alisema amejipanga kuonyesha umahiri wake katika mpambano huo baada ya kufanya hivyo wakati akiwa Sikinde dhidi ya Msondo kwenye ukumbi wa Diamond na kuwawehusha mashabiki wa muziki wa dansi nchini.

"Najua watu watataka kuona nafanya kitu gani dhidi ya bendi yangu ya zamani iliyonitangaza vyema, wasiwe na hofu waje Desemba 25 waone nini nitakachofanya TCC Club Chang'ombe," alisema Kambi.

Mpambano huo wa Sikinde na Msondo umeandaliwa na kampuni ya Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, Integrated Communications, CXC Africa na Salute5.

HATUMWI MTOTO DUKANI



UCHAMBUZI: YANGA Vs SIMBA

Na baraka mbolembole

Kocha mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic tayari ameonesha kufanya
mabadiliko katika upangaji wa kikosi chake, huku yule wa timu ya
Yanga, Ernie Brandts akiongeza suala la stamina kwa kikosi chake.
Logarusic alimpanga kiungo, Henry Joseph katika nafasi ya ulinzi wa
kati wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, wikiendi iliyopita na
mchezaji huyo alionesha kiwango kizuri.

 Kwa upande wa Yanga, kuwasili nchini na kujiunga na kambi ya timu
hiyo iliyopo katika hotel ya Protea kwa mshambuliaji, Emmanuel Okwi
kunataraji kuongeza ufanisi na makali zaidi safu ya mashambulizi ambayo mara kwa mara kocha, Brandts amekuwa akisema kuwa ni ' butu' na inayopoteza nafasi nyingi za kufunga, Okwi ni silaha ya hatari, huku
ushirikiano wake na washambuliaji Hamis Kizza na Mrisho Ngassa
ukisubiriwa kwa hamu.

MARA YA MWISHO...

April 20, 2003, mabao ya harakaharaka yaliyofungwa na kiungo, Salumu
Athumani, na mshambuliaji, Herry Morris katika dakika za 30 na 32, na
lile la dakika ya pili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili la
kiungo-mshambuliaji, Kudra Omary yaliweza kuipatia ushindi wa mabao 3-0 Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba, awali wiki mbili nyuma timu hizo zilifungana bao 1-1 katika mchezo wa kwanza wa kirafiki katika uwanja wa Uhuru. Simba ilitangulia kufunga kupitia kwa mshambuliaji Jumanne Shengo Tondola, na Yanga wakasawazisha kupitia kwa kiungo, Mrundi, Mwinyi Rajab.
MIAKA KUMI SASA.......

Kuongezwa kwa Okwi, na Said Dilunga katika kikosi cha Yanga kunaweza
kuwa kumeipa timu hiyo uimara zaidi katikati na bunduki muhimu mbele.
Lakini hakutasahihisha udhaifu mkubwa wa safu ya ulinzi. Kwa kuwa hata mabeki chaguo la kwanza wanapokuwa fiti, safu ya ulinzi huonekana kupwaya, waliruhusu mabao matatu dhidi ya Azam FC, na baadae Simba wakachomoa mabao yao matatu. Nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub
amekuwa akionesha dhahiri uwezo wake katika mchezo wa ' man to man',
ila si mzuri katika kujipanga na kuzuhia njia za hatari,

 David Luhende bado anajaribu kiwango ambacho kilimfanya kuwa mchezaji wakutumainiwa katika nafasi ya ulinzi wa kushoto, Mbuyu Twite ni namba mbilI mzuri, anashambulia na kuzuhia kwa haraka, mtaalamu wa mipira ya kurushwa na mwenye uwezo mkubwa kwa kupiga mipira iliyokufa. Kocha, Brandts mara nyingi alikuwa akipiga kelele kuwa anahitaji mshambuliaji, na golikipa, na tayari amewapata Okwi na Juma Kaseja, ila hakuonekana kudai nyongeza yoyote ya mlinzi, hasa yule wa kati. Ni Kelvin Yondan pekee anayeweza kucheza mfululizo katika kinachoweza kuitwa kiwango cha juu. Uwepo wa washambuliaji kama Betram Mombeki, Hamis Tambwe, Edward Christopher kunaweza kumkumbusha kocha huyo kosa alilolifanya.

SIMBA KAMA BARCELONA, YANGA KAMA REAL MADRID

Barcelona, mara zote huwa wanatoa matokeo ya kushangaza, pale wanapotabiriwa kufanya vyema huwa wanaanguka vibaya, na pele wasipotarajiwa huwa wanafanya maajabu. Wakiwa na mchezaji bora zaidi duniani, mahasimu wao wanao wachezaji wa bei mbaya ndani ya uwanja. Katika mchezo wao wa kwanza wa ' clasico', Real Madrid ilitota mbele ya Barca. Na sasa, pengine uwepo wa Haruna Niyonzima, Okwi, Hamis Kiza, Didier Kavumbagu, Twite, Kelvin, Nadir, Yanga wakawa na thamani kubwa zaidi ndani ya uwanja, kipesa. Ila Simba imekuwa timu yenye vipaji vinavyoendana na utamadunia wao wa mchezo wa pasi za chini chini.

Herry Joseph atasogea katika nafasi ya kiungo wa ulinzi ili kumpisha mlinzi, Donald Musoti kucheza na Joseph Owino. Uchezaji wa Amri Kiemba unaweza kuwa silaha, au maangamizi kwa Simba endapo atakuwa katika kiwango cha juu Simba itaendelea kuwa timu ile ile inayojiamini ikicheza na Yanga, na endapo itatokea kucheza kwa kiwango cha chini, timu itapotea uwanjani kama ilivyokuwa mwezi oktoba, wakati ule Jonas Mkude aliposhindwa kujiamini.

4-3-3

Timu ya Yanga inaweza kuwapanga kwa pamoja, Okwi, Kiza, na Ngassa katika safu ya mashambilizi jambo ambalo litawachanga walinzi wa pembeni wa Simba, ambao kwa sasa hawapo katika viwango vya juu. Simba inataraji kutumia mfumo huo pia, na uwepo wa kiungo Awadg Juma utaunganisha nguvu na viungo, Mkude na Henry, na kuwaacha Tambwe, Mombeki, na Kiemba katika safu ya mbele.

Kwa kuwa ni mechi ambayo Yanga wanaitumia kuipanga timu yao katika usawa, ni wakati mzuri wa kuwapanga pamoja, Chuji, Domayo na Niyonzima katika kiungo ili kuuchezesha mfumo huo kwa mwendo unaotakiwa, kasi na pasi za uhakika, fupi fupi au zile zenye urefu na macho ya kuangaza. Yanga wanao wachezaji hao na Simba kwa sasa ni timu inayotakiwa kujiendesha kwa mfumo wa 4-4-2 kwa kuwatumia mawinga kupiga krosi kwa washambuliaji wao ambao wanaonekana ni wazuri kwa mipira hiyo.

YANGA, JUMA KASEJA GOLINI

Ni kipa mzuri, kama ambavyo ameweza kudhihirisha hilo kwa kipindi cha miaka 11 sasa, Kaseja atasimama katika mchezo wake wa kwanza wa uhakika tangu mwezi, septemba alipoiwakilisha timu ya taifa katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Gambia. Aliruhusu mabao mawili wakati Yanga iliposhinda kwa mabao 3-2 dhidi ya KMKM ya Zanzibar, wiki iliyopita. Ataongeza kitu katika lango la Yanga na safu nzima ya ulinzi. Kuwakumbusha majukumu yao mara kwa mara walinzi, kucheza mipira ya kona na krosi ambayo iliwapa sare ya 3-3 katika mchezo wa mwisho wa mahasimu hao.

Thursday, October 17, 2013

PUMA YASITISHA MARA MOJA UDHAMINI WA SAFA.


Kashfa za upangaji matokeo zilizokuwa zikikikabili chama cha soka cha nchini Afrika Kusini ( SAFA ) zimepelekea kampuni ya PUMA iliyokuwa inazivalisha timu za Taifa za nchi hiyo  kusitisha mkataba mara moja.
Taarifa za PUMA kusitisha mkataba na SAFA zimekuja siku mbili baada ya benki ya Absa nayo kusitisha mkataba uliodumu kwa kipindi cha miaka 6.
Mnamo mwezi Disemba, uchunguzi wa Fifa ulibaini upangwaji wa matokeo kwenye baadhi ya michezo ya kujipima nguvu iliyoihusu Bafana Bafana wakati wa maandalizi ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010.
Kashfa hizo zilipelekea kusimamishwa kwa aliyekuwa raisi wa SAFA Kirsten Nematandani.

Monday, October 14, 2013

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAJITOKEZA KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA KUMBUKIZI YA NYUMBA YA MWL NYERERE ILIYOPO MAGOMENI MTAA WA IFUNDA KAMA ISHARA YA KUADHIMISHA SIKU YA MWL NYERERE TOKEA KUFARIKI KWAKE

 
 Bango linalosomeka Nje ya Nyumba ya Kwanza aliyowahi kuishi Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda barabara ya ifunda 60
 Hii ndio nyumba aliyoishi Hayati Baba Wa Taifa Mwl Julius Nyerere Kwa Kipindi Cha Miezi nane iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda, Barabara ya Ifunda namba 60 ambayo sasa imekuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Nyumba ya Mwl Nyerere
 Baadhi ya Wakazi wa Jiji La Dar Wakiwasili kwenye Nyumba aliyokuwa anaishi Hayati Mwl Nyerere Kipindi hiko kwaajili ya kujifunza na kufahamu historia yake japo kwa kifupi
 Wakazi wa Jiji la Dar Wakipata Maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wahudumu (hayupo pichani) wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda wakati walipofika leo kutembelea nyumba hiyo aliyokuwa akiishi Hayati Baba wa taifa Mwl Julius Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa ifunda
 Mmoja wa Kijana aliyefika kwaajili ya Kutembelea Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaani wa Ifunda Jijini Dar akiandika jina katika kitabu cha Wageni  mapema leo wakati alipotembelea Nyumba Hiyo leo
 Wakazi wa Jiji la Dar wakionyeshwa Chumba cha Watoto wa Kiume wa Hayati Baba Wa Taifa Mwl Juilus Nyerere na mmoja wa wahudumu wa Nyumba hiyo (hayupo pichani) wakati waliotembelea makumbusho ya kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere mapema leo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Jijini Dar
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akitoa maelezo ya Redio ya kwanza aliyopewa Mwl Nyerere kama zawadi na Malkia Elizabeth kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika kutembelea nyumba hiyo iliyotumiwa na Mwl Nyerere hapo Mhudumu wa nyumba hiyo akiwaonyesha wakazi wa jiji la Dar waliofika katika Nyumba hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda 
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akitoa maelezo kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika kutembelea nyumba hiyo iliyotumiwa na Mwl Nyerere hapo Mhudumu wa nyumba hiyo akiwaonyesha Rozari aliyokuwa akitumia Hayati baba wa Taifa Mwl julius Kambarage Nyerere 
 Mmiliki wa Lukaza Blog Josephat Lukaza pamoja na Wakazi wengine wakipata maelezo kutoka kwa Bi Theresia Gratta Makene (katikati) juu ya redio ya kwanza aliyopewa Mwl Nyerere Kama Zawadi kutoka Kwa Malkia Elizabeth 
 Wakazi wa Jiji la Dar wakiangalia baadhi ya Picha zilizobandikwa katika Kuta za Nyumba aliyokuwa akiishi Hayati Mwl Nyerere Kwa kipindi cha Miezi nane, Nyumba hiyo ipo Magomeni Mtaa wa Ifunda
 Baadhi ya watoto waliofika Katika nyumba hiyo Kwaajili ya Kuona vitu mbalimbali alivyowahi kutumia Hayati Mwl Nyerere vilivyopo katika Nyumba hiyo iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda
 Watoto waliofika mapema leo Katika Nyumba aliyowahi kuishi Hayati Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda wakiangalia vitabu vya Mwl Nyerere
Mmoja wa Wahudumu wa Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere Bi Latipha Juma akielezea juu ya baadhi ya vyombo alivyowahi kutumia Hayati baba wa taifa Mwl Nyerere wakati akiishi katika nyumba hiyo iliyopo Magomeni mtaa wa Ifunda.Picha zote na Josephat Lukaza wa 

KUELEKEA MECHI YA WATANI YANGA YAJICHIMBIA PEMBA


Baada ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika mjini Bukoba mwishoni mwa wiki, jana kikosi cha Young Africans kilirejea jijini Dar es salaam na leo asubuhi kilitua kisiwani Pemba ambapo kitakua kambini kwa muda wa wiki moja.

Young Africans inaweka kambi kisiwani Pemba ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika mchezo wake dhidi ya watani wa jadi Simba SC, ambapo kambi ya awali iliwafanya vijana wa jangwani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza 'Diego'.

Msafara wa watu 38 wakiwemo wachezaji wote 29 waliosajiliwa kwa ajili yakuichezea Yanga msimu huu na viongozi 9, watakua kisiwani pemba katika maandalizi ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga ili kujiweka katika mazuri ya kuongoza Ligi Kuu na baadae kuteteta tena Ubingwa wake.

Mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba leo asubuhi kwa ndege tatu za kukodi kikosi kimefanya mazoezi yake ya kwanza katika uwanja wa Gombani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mcezo dhidi ya Simba SC oktoba 20, 2013.

Ikiwa ni takribani siku sita kabla ya kupamba na Simba SC siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kikosi cha mholanzi kimeamua kuweka tena kambi katika visiwa hivyo tulivu kwa lengo la kusaka ushindi.

Kocha Mkuu Brandts amesema anatambua kikosi chake kinakabiliwa na mchezo mgumu, haswa ikizingatiwa wanapokutana watani wa jadi mechi huwa inakua ngumu sana lakini kwa sasa anakindaa kikosi chake ili kiweze kuendeleza wimbi la ushindi.

"Pemba ni sehemu nzuri, tulikuwepo huku mwishoni mwa msimu uliopita kwa ajili ya maandalizi dhdi ya Simba na tuliibuka na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa mazoezi mzuri na hali ya hewa ni nzuri vitatutaongeza chachu ya ushindi kufuatia kuwa sehemu tulivu" alisema Brandts

Wachezaji waliondoka kwenda Pemba ni:

Walinda Mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul.

Walinzi wa Pembeni: Mbuyu Twite, Juma Abdul, Issa Ngao, David Luhende na Oscar Joshua.

Walinzi wa Kati: Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani 'Cotton', Rajab Zahir na Ibrahim Job.

Viungo wa Ulinzi: Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo na Salum Telela na Bakari Masoud.

Viungo Washambuliaji: Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani na Hamis Thabit.

Washambuliaji wa Pembeni: Mrisho Ngassa, Saimon Msuva na Abdallah Mguhi 'Messi'

Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Reliants Lusajo na Shaban Kondo


Saturday, October 12, 2013

LIGI KUU KUENDELEA KUTIMUA VUMBI LEO

Ligi kuu Tanzania bara inaendelea tena leo katika viwanja tofauti wakati mabigwa watetezi Dar Young Africa wakiwa wageni wa Kagera Sugar .Wapinzani wao katika soka la bongo watakuwa Uwanja wa Taifa wakimenyana na Prison toka Mbeya  msimamo Simba wanaongoza wakiwa na pointi na pointi kumi na tano

Wednesday, October 09, 2013

PICHA ZA JEZI YA BRAZIL MAALUM KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA ZAVUJA.




Gazeti la Globo Esporte la nchini Brazil limelikisha picha za jezi 
zinazotaraji kutumika kwenye fainali za kombe la dunia 
zitakazofanyika nchini Brazil mwakani. Picha za jezi hiyo
 ambayo itatengenezwa na Nike zilitaraji kuzinduliwa mwezi
 Novemba mwaka huu.

Sunday, October 06, 2013

AJALI YAHUSISHA MAGARI MANNE KURASINI



Ajali imetokea  barabara ya Kilwa eneo la Ufundi Kurasini muda wa saa nne na nusu baada ya magari manne kugongana huku gari moja ya abiria (daladala) kuyumba na kuwagonjwa watoto watatu waliokuwa wamesimama wakisubiri kuvuka hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo  majeruhi walikimbizwa hospitali na wanaendelea vizuri.  (Picha na Betchezal Buha)